SHIRIKA la Ugavi umeme nchini (TANESCO) Mkoa wa Singida linatarajia kutumia zaidi ya shilingi milioni 549.5 kwa ajili ya kugharamia ukamilishaji wa miradi 23 ya umeme kwa kuboresha miundombinu ili kukidhi mahitaji wateja,kufanya ukarabati,kuongeza nguvu ya umeme pamoja na miradi mipya.
Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye ofisi za shirika hilo,Meneja wa TANESCO Mkoa wa Singida,Mhandisi Gamba Mahuggila amesema utekelezaji wa miradi hiyo yote mpaka sasa umefikia asilimia sabini. Aidha Mhandisi Mahuggila amebainisha kwamba kuna mradi wanaotegemea kuutekeleza na tayari wameshaufanyia uchambuzi wa kuhakikisha kwamba mji wote wa Singida unapatiwa umeme wa uhakika.Kwa mujibu wa Meneja huyo kuna sehemu 15 ambazo maeneo yake yanahitaji huduma za umeme na kuyataja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni pamoja na Kimpungua,NHC,VETA na mengine yanayokuwa kwa haraka yatapatiwa pia umeme wa uhakika katika siku za hivi karibuni.Kuhusu suala la Mkoa wa Singida kuongeza huduma kwa wateja,Meneja huyo ameweka bayana pia kwamba wameshafungua ofisi ndodgo ndogo kutekeleza agizo la serikali,kwenye maeneo ya Mji mdogo wa Shelui,Ndago na Mitundu. Mhandisi huyo hata hivyo amesema pamoja na kufungua ofisi kamili kwa kuziongezea uwezo kama vile Mkalama ambayo wameshapata Meneja na hivi sasa wanafanya utaratibu wa kuongeza wafanyakazi ili ofisi hiyo ya wilaya iweze kujitegemea kwa kila kitu na Ofisi ya Itigi baada ya kupata kiongozi wake muda wowote ule wataigeuza kuwa ofisi ya wilaya. Shirika la umeme Tanzania (TANESCO0 Mkoa wa Singida limeongeza wateja kutoka wateja 26,000 mwaka 2015 mpaka kufikia wateja 34,000 na wanatarajia kuwa na wateja 36,000 ifikapo julai,mwaka 2018.
0 Comments