WIZARA ya Fedha imepiga
marufuku kwa Maafisa masuhuli pamoja na wakuu wa taasisi wote nchini kutoingia
mikataba kwa watoa huduma na wakandarasi endapo watakuwa bado hawajapokea fedha
kutoka kwa mlipaji mkuu wa serikali,ili kuepuka kuzalisha madeni hewa yanayowezakuwa
kuwa mzigo baadaye kwa serikali.
Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango,Bi Ashantu Kijaji ametoa agizo hilo mjini Singida wakati alipokuwa
akizungumza na wafanyabiashara wadogo,wa kati na wakubwa wa Manispaa ya
Singida,kwenye ukumbi wa mikutano wa Mabula mjini Singida.
Aidha Naibu waziri huyo
amesema agizo hilo la kuzalisha madeni lilishatolewa na waraka wa serikali
kutoka kwa mlipaji mkuu,katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango kwamba mkuu
yeyote yule wa taasisi asiingie mkataba wowote na watoa huduma au wakandarasi
kama hawajapata fedha za kugharamia shughuli hizo.
Kwa mujibu wa Bi Kijaji
lengo la agizo hilo ambalo lilishatolewa tangu mwaka 2016/2017 ni kuhakikisha
kwamba maafisa masuhuli hao wanapoingia mikataba na Wakandarasi au Wazabuni
waweze kulipwa fedha zao ili waanze kazi.
Akijibu baadhi ya hoja za
wafanyabiashara hao,Mkuu wa wilaya ya Singida,Bwana Eliasi Tarimo ameweka
bayana sababu za jeshi la polisi kufanya upekuze kwenye nyumba za kulala wageni
wakati wa usiku kuwa ni pamoja na kuimarisha usalama kwa wananchi na kubaini
wahamiaji haramu wanaoingia nchini kiholela.
Kwa upande wao baadhi ya
wafanyabiashara wa Manispaa ya Singida,Bwana Valery Kimambo,pamoja na Naibu
Waziri kutoa ufafanuzi,lakini hakusita kuwasilisha kilio chao kuhusu riba kubwa
zinazotozwa na taasisi za kifedha kwa wakopaji katika taasisi hizo,na hivyo
kuomba kiwango hicho cha riba kipunguzwa.
Mmoja wa wafanyabiashara akiuliza juu ya kutokuwepo kwa ofisi ya afisa mausiano wa TRA mkoa wa singida. |
Mbunge wa Singida mjini Mh Mussa Sima akifafanua jambo katika mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa Rc Singida. |
0 Comments