WAVAMIZI WA KIMYAKIMYA MSITU WA UNYAMBUI ONDOKENI WENYEWE DC IGUNGA

Dc John Mwaipopo Igunga
Na,Jumbe Ismailly IGUNGA
MKUU wa Wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora,Bwana John Mwaipopo amewatangazia kiyama wananchi .wanaodaiwa kuvamia msitu wa hifadhi wa Halmashauri ya Unyambiu,uliopo katika Kijiji cha Mwajinjama,Tarafa ya Simbo,wilayani humo kuondoka mara moja kwenye hifadhi hiyo kabla serikali haijaanza kuchukua hatua dhidi yao.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa tahadhari hiyo baada ya kufanya ziara ya kushitukiza mwishoni mwa wili iliyopita kwa ajili ya kujionea jinsi gani msitu huo ulivyoharibiwa na baadhi ya wananchi wanaojihusisha na ukataji,uchanaji mbao pamoja na uchomaji wa mkaa.
Amefafanua mkuu wa wilaya huyo kwamba katika ziara hiyo kwenye msitu huo wenye ukubwa wa hekari 16,640,uliopo katika Kijiji cha Mwajinjama,wamefanikiwa kukamata misumeno miwili,baiskeli tano na tanuri mbili zilizopangwa kwa ajili ya kuchoma mkaa na kwamba tanuri mbili zilizokamatwa zina uwezo wa wa kutoa zaidi ya gunia mia mbili za mkaa huku watuhumiwa wakifanikiwa kukikimbilia kusikojulikana.
Aidha Bwana Mwaipopo amefafanua kwamba alishangazwa na kasi kubwa iliyoko katika msitu huo ya ukataji miti hovyo na uchomaji wa mkaa,hali ambayo amesema hatakuwa tayari kuuona msitu ukitoweka hovyo wakati uwezo wa kudhibiti upo.
Kwa upande wake Katibu tawala wilaya ya Igunga,Bwana Godslove Kawiche amesisitiza kwamba haiwezekani msitu uharibiwe kiasi kikubwa,huku Maofisa watendaji wa vijiji,wenyeviti wa vijiji na vitongoji wakiwepo hivyo kuamuru wakamatwe na kuwekwa mahabusu.
Nao baadhi ya wananchi wanaojishughulisha na biashara ya mbao pamoja na mkaa,Bwana Issa Rashidi,Bwana John Msumeno na Bwana Lucas Ipembe wamesema wanafanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha kwa kuwa hawana kazi zingine za kuwaingizia kipato nje na kazi hiyo.
Kwa upande wake Ofisa usafi na Mazingira wilaya ya Igunga,Bwana Fredrick Mnahela amesema kwa asilimia 60 msitu huo umeharibiwa kiasi ambacho juhudi za haraka zinahitajika ili kuunusuru msitu huo ambapo hata hivyo alionya kuwa hivi sasa mtu yeyote atakaye mkamata atafikishwa Mahakamani ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia hiyo.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments