MKUU wa Mkoa wa Singida,DK.REHEMA NCHIMBI ameahidi kuvifuta
vyama vya msingi vya wakulima wa zao la Tumbaku pamoja na Bodi ya Tumbaku ya
Mkoa wa tumbaku Manyoni endapo wakulima wa zao hilo watakosa soka la kuuzia
tumbaku yao waliyolima kwa mwaka 2016/2017.
Akifungua soko la zao la tumbaku kwa msimu wa kilimo wa
2016/2017 uliofanyika katika Chama cha Ushirika cha Msingi Isingiwe LTD
Mitundu,Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kwamba endapo wananchi hao watabaki na
zao la tumbaku ndani ya nyumba zao,mwenyekiti wa Bodi ya tumbaku ndiyo itakuwa
mwisho wa kuitumikia nafasi hiyo.
Hata hivyo Dk.Nchimbi hakusita kusisitiza juu ya upatikanaji wa
soko la zao la tumbaku za wakulima lipatikane ili kuondokana na maneno ya
minong’ono iliyozidi kwenye maeneo mbali mbali kwamba zao hilo linachachusha
hata asali.
Hata hivyo Dk.Nchimbi amewataka watendaji,hususani maafisa ugani
katika Halmashauri ya Itigi kujenga utamaduni wa kuishi na wakulima wa zao la
tumbaku badala ya kuwatembelea pale tu wanapohitaji michango ya shughuli mbali
mbali za mandeleo.
Katika risala ya wakulima wa zao la tumbaku wa vyama vitano
iliyosomwa kwenye sherehe hiyo na Mwenyekiti wa Chama Cha Ushirika cha Msingi
Isingiwe,Bwana Daud Ngayaula imevitaja vyama vitano vilivyolima zao la tumbaku
kwa msimu wa kilimo wa 2016/2017 kuwa ni pamoja na IsingiweAmcos, Manyanya Amcos,Idodoma
Amcos,Mtakuja Amcos na Umoja Amcos na kwmaba vyama hivyo vinatarajia kuzalisha
kilogramu 295,000 ambazo iwapo zitanunuliwa zote kwa wastani wa bei ya kitaifa
ya dola mbili za kimarekani kwa kilo,vyama hivyo vitapata dola 590,000 za zenye
thamani ya shilingi 1,298,000,000/= za kitanzania.
Hata hivyo Bwana Ngayaula hakusita kuzitaja baadhi ya changamoto
zinazovikabili vyama hivyo kuwa ni kupewa uzalishaji mdogo wa Makampuni na
kujitoa kwa Kampuni ya AOTTL kutonunua zao la tumbaku kwa msimu wa kilimo wa
2017/2018.
Naye Mwakilishi wa Makampuni yanayonunua tumbaku, Bwana Charles
Kizigha amesema katika siku ya kwanza ya ufunguzi huo wa soko,tumbaku
iliyonunuliwa ina thamani ya dola za kimarekani 575.786 sawa na shilingi za
kitanzania milioni 1,281,085.13 kwa bei ya shilingi 2,225.
0 Comments