Meneja wa TANROAD mkoa wa Singida Eng Leonard Kapongo akitoa ufafanuzi kwa mkuu wa mkoa.
|
Baadhi ya madaraja madogo madogo yaliyokwisha kamilika .
|
Mkuu wa mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akikagua ujenzi wa daraja hilo |
Wakala wa
barabara nchini (TANROADS) mkoa wa Singida, unatarajia kulipa fidia ya zaidi ya
shilingi milioni 153.2 kwa baadhi ya
wananchi wa kijiji cha Sibiti wilaya ya Mkalama, walioathiriwa na ujenzi wa daraja
kubwa la mto Sibiti.
Meneja wa TANROADS mkoa wa Singida, Leonard Kapongo, amesema hayo
wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo kwa mkuu wa mkoa
Dk. Rehema Nchimbi ambaye alifanya ziara ya kukagua ujenzi huo..
Amesema zaidi ya shilingi milioni 74.8 zimelipwa fidia kwa
wananchi waliotambuliwa katika awamu ya kwanza na kwamba malipo yaliyosalia ya
zaidi ya shilingi milioni 78.3 kwa wananchi waliotambuliwa katika tathimini ya
awamu ya pili, watafidiwa pindi fedha zitakapopatikana
Katika hatua nyingine, Eng. Kapongo amesema hadi kufikia machi
mwaka huu, maendeleo ya ujenzi huo, yamefikia asilimia 41.22
Amesema mkandarasi alipaswa kumaliza kazi kwa asilimia mia moja
april 2014 Lakini kutokana na mvua kubwa zilizonyesha mwaka 2013 na 2014,
zilisababisha mafuriko na kupelekea mkandarasi kusimama kwa kushidwa kufika
eneo la kazi.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa Dk. Nchimbi, ameipongeza kampuni ya
Kichina,Hainan International Ltd, kwa juhudi za kujenga daraja
hilo na maingilio ya barabara kwa upande wa mkoa wa Simiyu na mkoa wa Singida.
Wakati huo huo mkuu huyo wa mkoa, amekemea tabia ya baadhi ya
vibarua na wananchi, kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi vya wakandarasi
wanaojenga miradi inayogharimu fedha nyingi za serikali na za ufadhili.
Mradi huo utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 16.3
0 Comments