KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemfungia Hajji
Manara, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba kwa mwaka
mmoja kutojihusisha na masuala ya soka pamoja na kumpiga faini ya Sh. Milioni
9.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Wakili Jerome Msemwa amewaambia
Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam kwamba hatua hiyo imefikiwa baada
ya Manara kukutwa na makosa matatu dhidi ya TFF waliomlalamikia.
Msemwa ameyataja makosa hayo ya Manara dhidi ya mlalamikaji, TFF ni
kuituhumu na kuidhalilisha TFF, kueneza chuki za ukabila na la tatu kuingilia
utendaji wa shirikisho hilo.
Kwa makosa hayo yote,
anakumbana na adhabu ya kuwa nje ya masuala ya soka kwa mwaka mmoja na kulipa
faini ya Sh. Milioni 9 kabla ya kumaliza adhabu yake.
0 Comments