Klabu ya Barcelona
kwa sasa ina matumaini tele kufuatia beki wake mahiri Gerard Pique kuanza
mazoezi wakati wakielekea katika mchezo wao wa kesho wa nusu fainali ya mkondo
wa pili ya Kombe la Mfalme dhidi ya Athletico Madrid.
Beki huyo alilazimika kutolewa wakati wa mapumziko katika ushindi wa
mabao 3-0 waliopata Barcelona dhidi ya Athletic Bilbao Jumamosi iliyopita baada
ya kupata majeruhi ya msuli.
Meneja wa klabu hiyo Luis Enrique amesema majeruhi hayo ya Pique
yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na ratiba ngumu waliyonayo.
Hata hivyo, nyota huyo wa kimataifa wa Hispania alifanya mazoezi na
wenzake mapema leo na kuna kila dalili atakuwepo katika mchezo huo wa kesho
ambao Barcelona wanaongoza kwa mabao 2-1 waliopata katika mchezo wa mkondo wa
kwanza.
0 Comments