Na
Jenesta Zedekia
Mahakama ya wilaya ya
Singida imewasomea mashitaka Bw.Iman
Abdul (44)na Bi.Vaileth Mangoi(34)
wakikabiliwa na makosa 50 ikiwemo kula njama ya kutenda kosa na wizi wakiwa
watumishi wa umma.
Akisoma mashitaka
hayo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo wakili wa serikali Bi.Petrida Muta
amesema kuwa tukio hili lilitendeka kuanzia November,2013 hadi March 2014
ambapo mishahara ya watumishi 15 wakiwemo watoro,wastaafu na waliosimamishwa
kazi.
Aidha Bi.Muta amesema mishahara hiyo ilikuwa ikiingizwa kwenye Akaunti ya Iman
ambaye ni mshitakiwa namba moja kupitia Akaunti yake namba 50802503513 NMB tawi la Singida.
Amesema kwamba katika kutenda kosa la kula njama na wizi
akiwa ni mtumishi wa umma ni kinyume cha sheria kifungu cha 384 cha kanuni ya
adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Hadi hivi sasa kwa upande wa mashaidi wamefika watu 14
ambapo wamebakia mashaidi 5 ili kesi hiyo kukamilika kwa upande huo.
Jumla ya shilingi million ishirini na tano laki saba na kumi
na tatu elfu,mia sita kumi na moja nukta ishirini na saba ilikuwa akiingia
kwenye Akaunti ya mshitakiwa Namba moja ambaye ni Iman Abdul.
Hata hivyo hakimu wa
Mahakama hiyo Bi.Joyce Minde ameahirisha kesi hiyo hadi January,27,mwaka huu
itakapo kuja kwa ajili ya kusikilizwa.




0 Comments