Mh Tundu Lisu |
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amepandishwa kizimbani
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manne ya
uchochezi.
Wakili wa Serikali Kishenyi Mutalemwa aliwasilisha maombi
ya kupinga dhamana yaTundu Lissu kwa madai kwamba amekuwa na
mwenendo unaohatarisha amani si tu kwa wanajamii, bali hata kwake mwenyewe kwa
kuendelea kutoa maneno ya uchochezi.
Hakimu Huruma Shaidi, ametupilia mbali ombi hilo la serikali na
kumpa Tundu Lissu dhamana ya sh. Milioni 20
0 Comments