Washukiwa 13 wakiwemo wasanii
mashuhuri wamefikishwa mahakamani mjini Dar es Salaam Tanzania, baada ya ombi
maalamu la polisi kutaka wawekwe chini ya uangalizi kwa kipindi cha mwaka
mmoja.
Watuhumiwa hao wameamriwa na mahakama wawe chini ya uangalizi wa
polisi kwa mwaka mmoja ambapo pia wametakiwa kujidhamini kwa bondi ya shilingi
milioni 10 za Tanzania sawa na dola 4000.
Polisi nchini Tanzania wamekuwa wakiwashikilia watu zaidi ya 10
wakiwemo wasanii maarufu na polisi waliotajwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.
Miongoni mwa wale waliohojiwa, alikuwemo msaanii maarufu na miss
Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu, aliyeitikia wito wa polisi pamoja wasanii
wenzake kufika kwa mahojiano.
0 Comments