Nyimbo zilizokuwa zimepotea za
mwanamuziki Bob Marley, ambazo zilipatikana kwenye chumba cha chini cha hoteli
mjini London baada ya zaidi ya miaka 40 zimetengenezwa upya tena.
Kanda hizo za hali ya juu ni zile Bob Marley alirekodi moja kwa
moja, wakati wa tamasha zake za miji ya London na Paris kati ya mwaka 1974 na
1978.
Kanda hizo ni za nyimbo za No Woman No Cry, Jamming na Exodus.
Kwaza zilidhaniwa kuharibiwa kabisa kutokana na unyevu uliokuwa
eneo kanda hizo zilipatikana.
Marley ambaye aliaga dunia mwaka 1981, angekuwa na umri wa miaka
72 hii leo.
Kanda hizo zilipatikana kwenye hoteli ya Kensal Rise, kaskazini
magharibi mwa London, ambapo Bob Marley na bendi yake walikuwa wakiishi,
wakifanya tamasha zao barani Ulaya miaka ya sabini.
Kanda hizo ni kutoka kwa tamasha zilizofanyika maeneo la Lyceum
mjini London mwaka 1975, la Hammersmith Odeon 1976, na la Rainbow mjini London
mwaka 1977.
0 Comments