Spika John Boscow |
Spika wa Bunge la
Uingereza John Boscow amekosolewa kwa kupinga hatua ya rais Donald Trump
kuhutubia bunge la taifa hilo wakati wa ziara yake.
Mwanachama wa chama cha kihafidhina aliambia
BBC kwamba matamshi yake yamesababisha chuki huku mbunge mmoja akisema kuwa
hayafai huku wengine wakidai hafai kupendelea upande mmoja.
Bw Bercow alisema pingamizi dhidi ya ''ubaguzi
wa rangi na ule wa kijinsia'' zinapaswa kuangaziwa sana na wanachama wa bunge
hilo.
Mbunge wa Marekani Joe Wilson alisema kuwa ni
pigo kwa chama cha Trump cha Republican.
Mwandishi wa BBC wa maswala ya kisiasa
Eleanor Garnier amesema kuwa ni pigo la kidiplomasia kwamba rais Trump
hataruhusiwa kuhutubia bunge la nchi hiyo.
Mwezi uliopita waziri mkuu wa Uingereza
Theresa May alisema kuwa rais Trump amekubali mwaliko kutoka kwa malkia wa
Uingereza kwa ziara rasmi nchini Uingereza baadaye mwaka huu.
Lakini akizungumza bungeni siku ya Jumatatu
bw Bercow alisema kuwa anapinga rais Trump kuhutubia mabunge yote kama ilivyo
ada na viongozi wengine wa kimataifa.
Amesema kulihutubia bunge sio haki bali ni
heshima anayopewa kiongozi wa kimataifa.
Amesema kulihutubia bunge sio haki bali ni heshima anayopewa
kiongozi wa kimataifa.
''Nahisi kwamba pingamizi yetu dhidi ya ubaguzi wa kijinsia na
ue wa rangi na haua yetu ya kuunga mkono usawa na uhuru wa mahakama ni muhimu
sana na yanapaswa kupewa kipaumbele na wabunge wa Uingereza'', alisema.
0 Comments