Jared Kushner Mshauri wa Trump |
Rais mteule wa Marekani Donald Trump
amemteua mkwe wake Jared Kushner, kuwa mshauri mwandamizi wa Ikulu ya nchi
hiyo.
Kushner mwenye umri wa miaka 35 ambaye amemuoa binti mkubwa wa
Trump, Ivanka, alifanya kazi kubwa wakati wa kampeni za uchaguzi,
zilizomuwezesha Trump kushinda.
Majukumu ya kazi yake yanatarajiwa kuhusika na masuala ya sera
za nje na ndani ya nchi, ikiwemo masuala ya biashara na Mashariki ya Kati.
Uteuzi huo hauhitaji kuthibitishwa na bunge la seneti.
Lakini hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanahoji kama uteuzi huo
utakiuka sheria ya kupinga upendeleo wa undugu katika ajira.
Jared Kushner hata chukua mshahara kwa uteuzi huo wa Ikulu ya
Marekani na itampa nafasi ya kumfanya kuwa huru na maslahi ya shughuli zake za
kibiashara.
0 Comments