BAADA YA USHINDI YANGA YAPANDA KILELENI


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga leo wamepanda kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Mwadui.

Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam ulikua ni muhimu kwa Yanga kuibuka na ushindi ili kuitoa Simba ambayo imeshikia nafasi ya kwanza tangu mwanzoni mwa msimu.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia Obrey Chirwa alifunga mabao yote mawili ya Yanga leo na kuiwezesha timu hiyo ambayo inaiwakilisha Tanzania katika michuano ya klabu bingwa Afrika  ikifikisha pointi 46 ikiwa ni pointi moja mbele ya Simba

Katika mechi nyingine iliyopigwa leo Majimaji ya Songea iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara goli pekee la Kevin Sabatto

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments