George michael afariki dunia |
Mwanamuziki nguli mwenye asili ya
Uingereza, ambaye alijizolea umaarufu mnamo mwaka 1980 na kuwika ulimwenguni
kutokana na mtindo wake wa mahadhi ya pop, amefariki dunia.
George Michael amekufa akiwa na umri wa miaka hamsini na
tatu.Msemaji wa mwanamuziki huyo amearifu kwamba nguli huyo aliaga dunia akiwa
nyumbani kwake Oxfordshire.
Kundi la Wham lilijipatia umaarufu ulimwengu mzima na kupata
mafanikio makubwa kwa tungo zao kama 'Wake Me Up Before You Go-Go' na 'Careless
Whisper'
kundi hilo lilijizolea umaarufu na kuwa kundi la kwanza la
Magharibi kwa miondoko ya pop kufanya onesho la kimuziki nchini China.
Bendi hiyo iliposambaratika, George Michael aliendelea
kujizoelea umaarufu akiwa mwanamuziki wa kujitegemea.
Katika kipindi cha muongo uliopita alikuwa akisumbuliwa na
maradhi yasababishwayo na utumizi wa dawa za kulevya, ikiwemo kuendesha gari
kwa kasi na kupoteza mwelekeo na kuingia kwenye duka mjini London huku akiwa
amelewa dawa za kulevya.
0 Comments