Taifa la Tanzania limefutilia mbali
usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za taifa hilo
kinyume na sheria.
Waziri wa maswala ya kigeni wa Tanzania Augustine Mahiga
aliambia BBC kwamba meli hizo zilionekana hivi karibuni katika bahari hindi
eneo ambalo halipo mbali na Tanzania.
Hatahivyo hakutoa idadi kamili ya meli hizo.
''Meli za Korea Kaskazini zilipigwa marufuku na Umoja wa Mataifa
na hazikuruhusiwa kusafiri ama hata kutia nanga'',alisema Mahiga.
''Kwa hivyo meli hizi zimekuwa zikijaribu kutafuta njia kukiuka vikwazo
hivyo ili kuweza kuendelea na biashara zao,na mbinu moja ni kupeperusha bendera
za mataifa tofauti''.
Waziri huyo amesema kuwa malalamishi yametumwa katika serikali
ya Korea Kaskazini wakilaumu biashara hiyo ya ujanja.
''Shirika la kimataifa la maswala ya baharini pia limeelezewa
ili kuwakamata wamiliki wa meli hizo'',aliongezea Mahiga.
0 Comments