Mgombea wa urais kupitia tiketi ya
chama cha Democrat Donald Trump amesema kuwa atakubali matokeo ya uchaguzi wa
urais nchini Marekani ''iwapo atashinda'' .
Amesema kuwa atakubali matokeo ya moja kwa moja yasio na
udanganyifu wowote akiongezea kuwa ana haki ya kupinga matokjeo hayo iwapo
hayatakuwa na utata.
Alionekana katika mkutano mjini Delaware jimbo la Ohio
,akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya mjadala wa tatu wa urais dhidi ya
mpinzani wake wa chama cha Democrat Hillary Clinton.
Bwana Trump amekuwa akikosolewa kwa kusema kuwa hatakubali
matokeo ya uchaguzi huo.
Donald Trump alikataa kuahidi kukubali matokeo ya uchaguzi iwapo
atashindwa, katika mjadala wa mwisho wa urais dhidi ya Hillary Clinton.
"Nitakuambia wakati huo" alimwambia muendesha mjadala
Chris Wallace. Kwa siku kadhaa amedai kuwa kuna 'udanganyifu' katika uchaguzi
huo.
Mjadala huo wa televisheni Las Vegas uliendeleza uhasama katika
kampeni huku Trump akimuita Bo Clinton "mwanamke muovu".
Kura za kutafuta maoni zinaonyesha Trump poteza umaarufu katika
majimbo makuu baada ya kukabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono.
Mjadala huo wa mwisho wa umefanyika wiki tatu kabla ya siku ya
uchaguzi Novemba 8.
Wagombea hao walikataa kusalimiana kwa mikono kabla na baada ya
majibizano hayo ya kisiasa, hatua iliyofungua kile ambacho baadaye kiligeuka
kuwa mjadala wa kelele na kukatizana kauli.
Trump alitoa ahadi kwa wanachama wa Republican kuwateua majaji
wa mahakama ya juu zaidi wanaoegemea 'mrengo wa kihafidhina' watakaogeuza
sheria kuu inayohalalisha uavyaji mimba Marekani na kulinda haki za kumiliki
bunduki.
0 Comments