TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti
Boys imeshindwa kukata tiketi ya Fainali za Afrika mwakani Madagascar baada ya
kufungwa 1-0 na wenyeji Kongo - Brazzaville jioni jii Uwanja wa Kumbukumbu ya
Alphonse Massamba-Debat mjini Brazaville katika mchezo wa marudiano hatua ya
mwisho ya mchujo.
Kwa matokeo hayo, Serengeti Boys inatolewa kwa bao la ugenini
baada ya sare ya jumla ya 3-3, kufuatia kushinda 3-2 katika mechi ya kwanza
wiki mbili zilizopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji wa Serengeti Boys iliyo chini Mkurugenzi wa Ufundi,
Mdenmark Kim Poulsen, Kocha Mkuu, Bakari Shime na Kocha wa makipa na Muharami
Mohammed ‘Shilton’ wapo kwenye huzuni kubwa baada ya matokeo hayo mjini Brazzaville.
Hii inakuwa mara ya pili Serengeti Boys kuikosa kosa tiketi ya
fainali za Afrika baada ya mwaka 2005 kufuzu fainali za Gambia, kwa kuzitoa
Rwanda, Zambia na Zimbabawe, lakini ikaenguliwa kwa kashfa ya kumtumia mchezaji
aliyezidi umri, Nurdin Bakari aliyekuwa anachezea Simba SC wakati huo.
0 Comments