Okwi nje |
Hamisi kiiza yumo |
Juuko murushidi |
KOCHA wa Uganda, The Cranes, Milutin Sredojevic 'Micho' ametaja
orodha ya mwisho ya wachezaji 19 watakaomenyana na Togo mjini Lome Oktoba 4,
mwaka huu katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, akimtema mshambuliaji wa
zamani wa Simba na Yanga, Emmanuel Okwi.
Mserbia huyo, Micho amemchukua mshambuliaji mwingine wa zamani
wa Simba na Yanga, Hamisi Kiiza 'Diego' katika kikosi hicho ambacho kitamenyana
pia na Ghana Oktoba 7 katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia Urusi mjini
Tamale.
Kikosi kamili aklichoteua Micho kinaundwa na
makipa; Onyango Denis, Jamal Salim na Ochan Benjamin
Mabeki: Wadada Nicholas, Iguma Denis, Isinde Isaac, Juuko
Murushid, Ochaya Joseph na Walusimbi Godfrey.
Viungo: Wasswa Hassan, Kizito Geoffrey, Aucho Khalid, Mawejje
Tony na Oloya Moses.
Washambuliaji: Kizito Luwagga, Miya Faruku, Massa Geoffrey,
Kiiza Hamis na Sentamu Yunus.
Timu hiyo iliyofanya mazoezi kwa mara mbili jana na leo Uwanja
wa Taifa wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda inatarajiwa kuondoka usiku wa
leo kwa ndege ya Ethiopia.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Darius
Mugoye atasafiri na timu hiyo kama Mkuu wa msafara na timu hiyo inaondoka baada
ya kupewa Sh. Milioni 6620 za Uganda na Rais wa Jamhuri ya nchi
hiyo, Yoweri Kaguta Museveni kusaidia maandalizi dhidi ya Ghana.
Rais Museveni alimpigia simu binafsi, Rais wa FUFA, Mhandisi
Moses Magogo jana kumpa ujumbe huo auwasilishe kwa wachezaji kuelekea mechi
hiyo ya nyumbani.
Wachezaji wanaotarajiwa kusafiri kutoka Kampala ni Patrick
Ochan, Wadada, Kizito Geoffrey, Ochaya, Wasswa, Aucho na Tony Mawejje.
Denis Onyango atawasili kesho na kuunganisha ndege kwenda Lome,
Togo. Sentamu na Luwagga wataungna na timu mjini Lome wakati wachezaji
wengine wataungana na timu Addis Ababa usiku wa leo kuunganisha safari ya
kwenda Lome.
0 Comments