Jeshi la polisi mkoa wa Singida, linamshikilia askari mgambo
mwajiriwa wa hospital ya mkoa, Emmanuel Daghau kwa tuhuma ya kutoa taarifa za
uongo juu ya maiti kufufuka ikiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha
hospitali ya hiyo.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SSP Mayala Towo amesema
tukio hilo limetokea septemba 30 mwaka huu, majira ya alasiri katika hospitali
ya mkoa ambapo septemba 29 mwaka huu Rahel Erasto (28),alifikishwa
katika hospitali hiyo ya mkoa,kwa ajili ya kupata huduma ya kujifungua salama.
Aidha kamanda amesema kutokana na sababu za kitabibu Rahel,
alishindwa kujifungua kwa njia ya kawaida na hivyo ikalazimika kufanyiwa
upasuaji ambapo mtoto wa kiume alitolewa akiwa hai Lakini mama kwa bahati mbaya
alifariki dunia usiku wa saa saba septemba 30, 2016
Amesema kuwa baada ya Rahel kufariki dunia, mwili wake ulipelekwa
Chumba cha kuhifadhi maiti ambapo kesho yake, ndugu walijikusanya
eneo hilo wakijadiliana namna ya kuuchukua mwili kwa ajili ya mazishi Ndipo
alijitokeza mlinzi Daghau na kuwaeleza kuwa ndugu yao huyo, alifariki
kutokana na uzembe kwani akiwa kwenye doria za kawaida, alisikia marehemu
akipiga chafya na aliposongelea dirishani, alimwona akiwa amefufuka.
Hata hivyo Kaimu mganga mkuu wa mkoa, Dk.Ramadhani Kabala amekiri
kuwepo kwa taarifa hizo na kudai kwa sasa mwili wa marehemu unaendelea
kufanyiwa uchunguzi ili kutambua kama kweli Rahel alifufuka na kupiga chafya
akiwa ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Singida, mhandisi Mathew
Mtigumwe amesema amepokea taarifa hiyo na kwamba zipo timu mbili zinaendelea na
kuchunguzi ili ukweli uweze kubainika.
0 Comments