MAHAKAMA YAPIGA STOP MKUTANO WA DHALULA WA MANJI



MKUTANO Mkuu wa dharula wa klabu ya Yanga uliokuwa ufanyike jumapili umezuiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kufutia kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo.

Kwa mujibu wa hati ya agizo halali la Mahakama, uongozi wa Yanga umezuiwa kufanya Mkutano huo baada ya kesi iliyofunguliwa mahakamani hapo dhidi ya Mwenyekiti wa klabu, Yussuf Manji na Kampuni ya Yanga Yetu.


Manji anatarajiwa kuzungumza na Waandishi wa Habari leo mchana kutolea ufafanuzi hilo.

Ajenda kuu ya Mkutano huo ni kupitisha Baraza la Wadhamini la klabu hiyo pamoja na kuondoa Mjumbe mmoja na kuweka mpya.

Na hayo yanafuatia Baraza la Wadhamini kuikodisha timu kwa kampuni ya Yanga Yetu kwa miaka 10, baada ya wanachama kuafiki ombi la Mwenyekiti wao, Yussuf Manji katika Mkutano wa Agosti 6, mwaka huu.



Yanga ilipanga kuwa na Mkutano wa dharula kesho Uwanja wa Kaunda, uliopo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam. 



Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments