Mfanyakazi mmoja wa
reli alisema kuwa kampuni hiyo iliongeza mabehewa nane kwa treni hiyo inayokuwa
kwa kawaida na mabehewa tisa, ili kumudu idadi kubwa ya abiria waliotaka
kusafiri. Maafisa wa reli waliiambia redio ya taifa kuwa treni hiyo ilikuwa na
abiria 1,300 badala ya idadi yake ya kawaida ya watu 600.
Mwandishi wa habari
wa Shirika la Reuters aliyekuwa akisafiri kwenye behewa moja karibu na sehemu
ya mbele ya treni hiyo alisema alisikia mshindo mkubwa. "niliangalia nyuma
na mabehewa yaliyokuwa nyuma yetu yaliacha reli na kuanza kubingiria. Kulikuwa
na moshi mkubwa" alisema.
Mhudumu mmoja wa
kampuni ya Camrail, ambayo inasimamiwa na kampuni ya Ufaransa ya Ballore
akizungumza katika eneo la ajali alisema kuna miili ya wanawake, na watoto na
kuongeza wafanyakazi wenzake watatu ni miongoni mwa watu waliofariki. Joel
Bineli, abiria aliyekuwemo kwenye treni hiyo iliyoanguka aliambia Reuters kuwa
kulikuwa na miili mingi iliyokatika vipande vipande kwenye barabara ya reli.
Camrail ilisema
iliyatuma makundi ya watu kwenda katika eneo la ajali na kuwa waliojeruhiwa
wamepelekwa hospitalini. Wengine walisafirishwa kwa magari hadi Douala.
Barabara nyingi za reli katika Afrika Magharibi na Kati zina sifa ya ukarabati
duni na kushindwa kukidhi kanuni za usalama. Matukio ya matreni kuwacha reli
hutokea mara kwa mara.
0 Comments