Mkoa wa Singida umebainika kuwa na kiwango kidogo zaidi cha
udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, unaosababishwa na
utapiamlo ikilinganishwa na kiwango hicho kitaifa.
Utafiti uliofanywa mwaka jana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, wazee na watoto kuhusu suala la afya ya mama na mtoto unaonesha
kuwa wakati kiwango cha kitaifa kwa utapiamlo ni asilimia 34, katika mkoa wa
Singida ni asilimia 29.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dk Angelina Lutambi amesema
hayo hivi karibuni katika hafla ya ufunguzi wa mkutano wa wadau wa Ushawishi wa
Lishe ulioandaliwa na Asasi ya Mtandao wa Kiraia (Ngonedo) ya mkoani Dodoma.
Hata hivyo, Dk Lutambi amesema kiwango hicho si cha kujivunia
kwa kuwa udumavu ni moja ya tatizo kubwa la lishe nchini, huathiri nguvu kazi
na huchangia kwa kiasi kikubwa kuathiri uchumi wa kaya na jamii kwa ujumla.
0 Comments