WILFRED KIDAO ASHUHUDIA FAINALI YA LIGI YA WANAWAKE SINGIDA, ATOA PONGEZI KWA VIONGOZI

 



Katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Nchini TFF Wilfred Kidao wa pili kutoka kushoto mwenye suti ya kijivu akiipigia makofi timu ya wanawake ya Ipembe baada ya kuibuka washindi wa Pili katika fainali ya ligi hiyo.



Na Mwandishi wetu

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wilfred Kidao, ameshuhudia fainali ya Ligi ya Wanawake Mkoa wa Singida na kutoa pongezi kwa viongozi wa soka la wanawake kwa mchango wao katika maendeleo ya mchezo huo.

Kidao alimpongeza Mwenyekiti wa Soka la Wanawake Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Yagi Mairidi Kiaratu, kwa juhudi zake za kuendesha ligi hiyo kwa miaka mitano mfululizo. Vilevile, alimpongeza Mwenyekiti wa Soka Mkoa wa Singida, Hamisi Kitila, kwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza mpira wa miguu mkoani humo.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments