MKUU WA MKOA WA SINGIDA ATOA WITO WA USHIRIKIANO KATI YA JAMII NA JESHI LA POLISI

 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akiongea na Makamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida na wageni waalikwa.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida SACP Armon Kakwale akiongea katika Maadhimisho hayo.




       Maonesho Mbalimbali katika viwanja vya Bombadia Mjini Singida katika Maonesho hayo.




Zawadi mbalimbali zikitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida kata Sherehe fupi iliyofanyika jioni katika ukumbi wa Uhasibu.




                        

                             Viongozi na wageni mbalimbali wakipata chakula kwa pamoja.


Singida,

 01 Machi 2025 

 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amehimiza jamii kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa ushirikiano wa dhati ili kukomesha uhalifu na kuhakikisha sheria zinaheshimiwa bila shuruti. Amesema mshikamano huo utasaidia kupunguza mzigo wa majukumu yasiyo ya lazima kwa Jeshi hilo.

Dendego alitoa wito huo alipokuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Familia ya Jeshi la Polisi, yaliyofanyika katika viwanja vya Bombadia, Manispaa ya Singida. Alibainisha kuwa ni jambo la kutia moyo kuona wananchi na Jeshi la Polisi wakishirikiana katika kulinda amani na usalama wa jamii.

Awali, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP Amorn Kakwale, alimkaribisha Mkuu wa Mkoa na kueleza changamoto inayowakabili askari kuhusu upatikanaji wa viwanja kwa ajili ya kujenga makazi binafsi. Alitoa wito kwa serikali na mamlaka husika, zikiwemo halmashauri, kutafuta suluhisho la tatizo hilo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Dawati la Jinsia wa Jeshi la Polisi, Amina Faki, alieleza kuwa ukatili dhidi ya watoto umeongezeka mkoani Singida kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo imani za kishirikina kwa lengo la kutafuta utajiri, migogoro ya kifamilia inayochochewa na unywaji wa pombe na umasikini, pamoja na wazazi kutochukua majukumu yao ipasavyo.

Maadhimisho haya yamelenga kuimarisha mshikamano wa familia za askari polisi na kuongeza ari katika utekelezaji wa majukumu yao ya kulinda raia na mali zao.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments