Meneja mpya wa Manchester United Ruben Amorim anatamani
kumsajili winga wa Wolves wa Algeria, Rayan Ait-Nouri, 23.
The Red Devils pia wanavutiwa na Christopher Nkunku wa Chelsea
lakini wanaweza kukabiliwa na ushindani kutoka kwa Borussia Dortmund kwa mshambuliaji
huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27.
Newcastle wanavutiwa na mshambuliaji wa Bournemouth Mghana
Antoine Semenyo, 24, lakini hawana uwezo wa kumnunua mwezi Januari hadi pale
wachezaji wengine watakapoondoka .
Fulham na Leicester wanatazamia mkataba wa mkopo mwezi Januari
kumnunua mshambuliaji wa Brighton na Jamhuri ya Ireland, Evan Ferguson, 20.
0 Comments