RC SINGIDA HALIMA DENDEGO AONGOZA WANANCHI KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA.

 

mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akionesha kadi yake baada ya kuboresha taarifa yake kwenye daftari la mpiga kura.




Katibu tawala Mkoa wa Singida Dkt Fatma Mganga akiwa na furaha baada ya kuboresha taarifa zake kwenye daftari la mpiga kura.


Mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe na Katibu tawala wilaya ya Singida Naima Chondo pia wamefika katika kituo hicho kupata huduma hiyo.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida naye amefika katika kituo cha kujiandikisha cha Bomani Manispaa ya Singida na kuboresha taarifa zake katika Daftari la wapiga kura.

SINGIDA

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, ameshiriki katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuwahimiza wananchi kujitokeza katika vituo vyao ili kuboresha taarifa zao.

RC Dendego amesema hayo leo, Septemba 25, 2024 wakati zoezi hilo likianza rasmi kwa Mkoa wa Singida na likitarajia kudumu kwa siku saba mpaka Oktoba Mosi mwaka huu. Kiongozi huyo aliweza kujiandikisha katika Kituo cha Chuo cha Wasioona.

"Tunamshukuru Mungu tumeamka salama na kuanza zoezi hili muhimu la kuboresha taarifa,"

Mhe. Dendego alitoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maandalizi bora yaliyofanywa, yanayoweza kuwasaidia wananchi kupata kadi zao za mpiga kura kwa urahisi.

Aidha alisema kuwa Mkoa wa Singida umeotewa kuwa na ongezeko la takriban wananchi laki mbili (200,000), hivyo aliwataka wakazi kujitokeza kwa wingi ili kujiandikisha na kuboresha taarifa zao.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments