WANANCHI WEKENI AKIBA SEHEMU SALAMA -BOT

 

Afisa Mchambuzi mwandamizi maswala ya fedha Gloria Chellunga Bank kuu akitoa ufafanuzi juu ya maswala ya akiba na mikopo.



Maofisa wa bank kuu wakitoa maelezo mafupi kwenye banda la bank kuu katika maonesho ya mifuko na program za uwezeshaji wananchi kiuchumi. 

SINGIDA

Wito umetolewa kwa wananchi kuweka akiba au fedha sehemu zilizo rasmi kama taasisi za kifedha zilizo sajiliwa na kusimamiwa na mamlaka za serikali ili kuweka historia ambazo zitawasaidia hata katika kupata mikopo.

Hayo yameelezwa na mchambuzi mwandamizi wa maswala ya fesha kutoka benki kuu ya Tanzania Gloria Chellunga katika maonesho ya saba ya mifuko ya program za uwezeshaji wananchi kiuchumi kanda ya kati yaliyozinduliwa leo Mkoani Singida katika kiwanja cha Bombadia.

Amesema wananchi wanapowekeza fedha zao sehemu sahihi zinazosimamiwa na kutambuliwa na mamlaka za serikali pamoja na kupata riba lakini itawarahisishia kupata mikopo pindi wanapohotaji kwa kuangalia historia ya kuweka fedha.

Aidha Chellunga ameeleza kuwa benki kuu inatoa dhamana za mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kupitia benki na taasisi wanazoombea mikopo hivyo wananchi watembelee katika maonesho hayo ili kupata elimu na kuweza kusaidiwa kupata mkopo.

Amefafanua kuwa benki kuu inasimamia mifumo yote ya kifedha na ni taasisi inayohudumia wananchi wote na sio wafanya biashara wakubwa kama baadhi ya watu wanavyoamini.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments