Ikungi
Kampuni ya General Traders yenye
makao makuu ya Dar es salaam imejikita kununua zao la dengu kutoka kwa wakulima
wadogo wilaya ya Ikungi Mkoani Singida kupitia vyama vidogo vya
ushirika vilivyopo vijijini na kuliuza zao hilo kwenye makampuni makubwa nje ya
nchi.
Kampuni hiyo ambayo imeweka ofisi
zake kwenye AMCOS tatu Mnang’ana Amcos, Muungano AMCOS na GREEN LUGO kuanzia
mwezi AUGUST mwaka huu tayari inayo tani 987 na kilo 666 ambazo inatarajiwa
kuingizwa sokoni kwa njia yam nada na inaendelea kukusanya dengu kutoka sehemu
mbalimbali Ikungi kupitia vyama vya ushirika.
Kwa mujibu wa meneja wa kampuni
hiyo alioko ofisi za AMCOS tatu Mnang’anaa Hamid mgeni
amesema kampuni yake inasimamia AMCOS tatu wilaya
ya Ikungi kununua zao la dengu kutoka vyama vidogo vya
usharika na kuuza dengu kwenye makampuni yanayonunua zao hilo na kulisafirisha
nje ya nchi kwa mauzo.
Hamidi amesema mpaka sasa kampuni
yake imeweka mikakatio ya kununua zao hilo kwa bei nzuri kutoka vyama vidogo
vya usharika ikilenga kuwainua wakulima wakati huo huo kuweka
walanguzi kuingia vijijini kwa wakulima kulangua kwa bei ndogo
inayowapa wakulima hasara.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo
Ramadhani Kilima hakluweka kupatikana ili kueleza kiasi cha fedha
kilichopatikana kutokana na mauzo ya minada minne iliyofanyika kwenye AMCOS
zake ambapo katika mnada wa kwanza dengu iliuzwa sh 2,414/=kwa kilo, mnada wa
pili dengu iliuzwa sh 1900/= kwa kilo na mnada iliobakia dengu iliuzwa sh
1,870/= kwa kilo moja.
akitoa historia ya jengo la ghala
la AMCOS Mnang’ana mwenyekiti wa AMCOS hiyo Mussa Ramadhani amesema jengo lake
linahifadhi tani 3,000 za mazao ya wakulima yanayouzwa kutoka vyama vidogo vya
ushirika vijijini mahali walipo jengo hilo lina ofisi mojam, ukumbi, mizani
mbili na ghala kuu na limejengwa na Farm Africa mwaka 2022 kwa
kushirikiana na VN-Women kupitia vifadhili wa shirika la KOICA KUTOKA NCHI YA
Korea.
Aidha mkurugenzi wa Halmashauri
ya wilaya ya Ikungi Justice KIjazi amesema maghala ya AMCOS Ikungi Mnang’ana,
Muungano na Green Lugo yamejengwa kutoa huduma za kuhifadhi mazao ya wakulima
ili baadae wajewauze kwa bei nzuri kutoka masoko yake kukwepa walanguzi.
Kijazi amesema Maghala kama hayo
ni sehemu sahihi na yenye uhakika wa kutunza mazao ya wakulima iliyawe salama
kuepuka kushambuliwa na wanyama na wadudu kutokana na uhifadhi mbovu vipindi
vya mavuno kwa sababu wakulima wengi wanahifadhi mazao yao nje ya nyumba kwa
vihenge na wakati huo huo kuepuka sumu kuvu.
Diwan wa kata ya
Sepuka Halima Ngimba anaishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na
Raisi Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea maghala matatu ya
kuhifadhi mazao ya wakulima wa wilaya ya Ikungi ili yauzike kwa utaratibu unaotakiwa
na serikali na kwa bei wanayotaka wao kukwepa walanguzi kupitia stakabadhi
ghalani.
Halima ametoa ombi kwa wizara ya
kilimo kwa waziri mwenye dhamaa kuliweka zao lao la alzeti kuingizwa kwenye
utaratibu wa stakabadhi gjhalani maana ndio sehemu sahihi kwa kuhifadhi na
uuzaji kwa sauti ya pamoja ya wakulima kukwepa walanguzi.
0 Comments