WAZIRI AWESU ATOA SAA 72 MBEYA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso ametoa saa 72 kuanzia leo tarehe 24 Septemba 2018 kwa mkandarasi wa mradi wa maji wa Galijembe mkoani Mbeya kurudi katika ene la ujenzi na kukamilisha kazi hiyo kabla ya kutafutwa.

Mhe. Aweso ametoa wito kwa mkandarasi baada ya kukagua mradi huo na kupokea mrejesho kutoka kwa wananchi wa Kijiji cha Galijembe kusubiri mradi huo kwa muda mrefua. Mradi wa Galijembe ulianza kutekelezwa mapema mwaka 2013, hata hivyo bado haujakamilika na mkandarasi hayupokatika eneo la kazi.

Mhe. Aweso pamoja na kutoa wito huo amesema mhandisi wa maji yeyote nchini ambaye anashindwa kufuatilia maendeleo ya miradi ya maji na kutoa taarifa kwa wakati hafai katika kazi hiyo. Amesema jambo la msingi ni kuhakikisha kazi inafanyika kwa ubora na wakati ili wananchi wapate huduma ya majisafi na salama.

Mhe. Aweso amesisitiza hawezi kukubali kuona mhandisi wa maji yupo na wakati huohuo mkandarasi anaharibu kazi, hivyo ameagiza wote waliohusika na mradi huo toka ulipoanza waitwe ili kujua ukweli wa mradi kutokamilika kama ilivyopangwa katika mkataba.
Waziri Aweso amesema wahusika wote wanahitajika kwasababu kumbukumbu zinaonyesha mkandarasi kalipwa kiasi cha Shilingi Milioni 263 kati ya Milioni 299, thamani ambayo ni tofauti na uhalisia wa mradi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Maji na Umwagiliaji

24.09.2018

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments