Semina elekezi
ya mafunzo ya msingi kwa lugha ya Alama ili kujenga mwamko kwa watumishi
wa serikali.
Semia hiyo inayowakutanisha watumishi wa serikali
kutoka jeshi la Polisi,Mgereza na Mahakama ya wilaya ya singida mijini huku mgeni rasimi katika semina hiyo ya siku
tano inayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa KBH Hotel Mjini Singida alikuwa
ni mkuu wa mkao wa Singida na kuwakilishwa na Mganga mkuu wa mkoa wa singida Dr
Victoria Ludovic .
Akisoma Risala mbele ya mgeni rasimi mkurugenzi wa
Shirika la BETHEL BAPTIST DEAF CHURCH (BBDC) lenye makoa yake makuu
mijini Dodoma Bw Frank Laurent amesema kuwa shirika hilo linampango wa
kuendelea kutoa elimu zaidi kwa watumishi wa ngazi mbali mbali nchini.
Akijibu risala kwa niaba ya mkuu wa mkoa Dr Rehema
Nchimbi iliyosomwa na mkurugenzi wa shirika la hilo Mganga mkuu wa mkoa wa
Singida Dr Victoria Ludovic alianza kwa kulipongeza shirika hilo .
Nao baadhi ya washiriki wa Semina hiyo Hakimu mfawidhi
wa mahakama ya wilaya ya singida bi Aristida Tarimo, Afisa ustawi wa jamii
manispaa bi Judith Misango na Afisa polisi kitengo cha dawati singida Bw Kenedy
Singlanda kwa nyakati tofauti wameshukuru kupata mafunzo hayo.
0 Comments