Miezi minne baada ya ulimwengu kubaini kuhusu kuwachana kwa nyota wa muziki wa bongo Diamond Platinumz na mpenziwe Zari Hassan, msanii wa muziki wa Injili nchini Kenya Alex Apoko ,maarufu Ringtone ameonyesha hamu ya kumchumbia mama huyo wa watoto watano.
Ringtone anayejulikana
kwa wimbo wake 'Tenda Wema' aliyeimba na msanii wa Tanzania Christine Shusho
anasema kuwa yeye ndio suluhu kwa matatizo ya kimapenzi ambayo yamekuwa
yakimzonga mfanyibiashara huyo wa Uganda.
Msanii huyo sasa
amemtaka mfanyibiashara huyo kutokubali kumrudia Diamond Platinumz na badala
yake kukubali uchumba wake kwa lengo la kumtumikia Mungu.
''Diamond
aniwachie Zari, Zari ni wangu wa Moyoni, atuwache tumtumikie Mungu'', alisema
Ringtone alipotembelea afisi mpya za BBC jijini Nairobi.
Msanii huyo anasema
kwamba aliota ndoto siku ambayo wawili hao waliachana ambapo anadai kumuona
Zari.
Alipoulizwa kwa nini unamtaka Zari,
Ringtone alikua mwepesi wa kujibu akisema kuwa ni mwanamke mrembo na mpenda
biashara.
Anasema kwamba kwa kuwa amepiga hatua katika safu ya muziki
anadhani kwamba Zari atamsaidia pakubwa kuendeleza biashara zake iwapo
watafunga ndoa.
Vilevile amesema kuwa mfanyibiashara huyo wa Uganda ambaye kwa
sasa amekita kambi nchini Afrika Kusini hafai kuumizwa na kuvunjwa moyo mara
kwa mara.
Aidha amedai kwamba yuko tayari kuwakubali wanawe mfanyibiashara
huyo akisema watu kutoka familia yake wanapenda watoto na kwamba nyumba yake
yenye vyumba kumi ina nafasi kubwa ya kumkaribisha Zari na wanawe.
Matamshi ya mwanamuziki huyo yanajiri wiki chache baada ya Zari
kuzuru nchini Kenya kwa hafla ya kampeni ya kukabiliana na ugonjwa wa saratani.
Wakati wa Ziara hiyo
Ringtone alitaka kumchumbia Zari kupitia gari jipya aina ya Range Rover lakini
raia huyo wa Uganda alinukuliwa na vyonbo vya habari akilikataa na kusema kuwa
alikuwa amenunua gari kama hilo wiki moja iliopita.
''Kwa kweli gari
nililomnunulia bado lipo na sijaamua nitalifanyia nini, mimi najua Zari
ananipenda lakini ni nyinyi wanahabari ambao munampatia shinikizo kubwa. Najua
kila akiamka ananitazama katika akunti yangu ya Instagram'', alisema nyota huyo
wa muziki wa Gospel.
Akihojiwa na baadhi ya
vyomnbo vya habari nchini Kenya Zari alikana kuwahi kuwasiliana na msanii huyo
akiongezea kwamba hana haja naye na kwamba anataka kutumia wakati wake mwingi
kuendeleza biashara zake na kuwaangalia wanawe.
Zari na Diamond
waliwachana siku ya wapendwanao ya Valentine mwaka huu baada ya kudai kwamba
nyota huyo wa muziki wa bongo amekuwa akimdhalilisha kupitia uhusiano na
wanawake wengine.
0 Comments