Shirikisho la Soka
Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limekubali maombi ya Yanga kujiondoa katika
mashindano ya KAGAME baada ya kutuma barua iliyoeleza kuomba kujitoa
Yanga ilituma barua
kupitia TFF ikiomba kujiondoa ili kuwapa nafasi wachezaji wake mapumziko kwa
ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia
FC ya Kenya.
Barua hiyo ilieleza
kuwa ratiba ya michuano imekuwa si rafiki kwao na itakuwa inawabana sababu
wanapaswa kuwajibika kwenye mashindano ya shirikisho pia wachezaji wake wengi
hawana mikataba.
Kutokana na maombi
hayo, CECAFA wamemua kuuwaalika Vipers SC ya Uganda kuchukua nafasi ya Yanga
ambapo katika kundi C wataungana na Simba, Dakadaha ya Somalia na St. George ya
Ethiopia.
Michuano hiyo
inatarajia kuanza kurindima June 28 mwaka huu na kumalizika Julai 13 2018.
0 Comments