Paka mmoja maarufu ambaye anadaiwa
kuwa na uwezo wa kipekee wa kutabiri ametabiri mshindi wa mechi ya kwanza ya
Kombe la Dunia nchini Urusi.
Kwa mujibu wa paka huyo aliyepewa jina Achilles, Urusi ndio
watakaoshinda mechi hiyo.
Achilles, paka wa rangi nyeupe ambaye ni kiziwi, hubashiri
mshindi kwa kuchagua katika ya bakuli mbili ambazo zimewekwa bendera za mataifa
yanayocheza.
Paka huyo ni miongoni mwa paka wanaofugwa kukabiliana na panya
katika makumbusho ya Hermitage mjini St Petersburg, ingawa sasa ana majukumu
hayo mapya.
Anadaiwa kubashiri kwa ufasaha
mshindi wa Kombe la Mashirikisho mwaka 2017.
Paka huyo alitoa utabiri wake wa sasa Jumatano.
"Achilles yuko tayari kutumiwa kwa umma na huwa hana
wasiwasi kuwa eneo lenye watu wengi," anasema daktari wa mifugo Anna
Kondratyeva, ambaye humtunza.
Hata hivyo, ubashiri wake haukutimia kwani Urusi ndio
waliotunukiwa hadhi hiyo.
Paul alifariki Oktoba mwaka 2010 kifo cha kawaida kulingana na
hifadhi ya Oberhausen nchini Ujerumani.
Watabiri wengine
Wanyama wengine wametambulishwa kwa umma wakiaminika kuwa na
uwezo wa kumrithi pweza Paul, akiwemo nungubandia, yaani guinea pig, kwa Madame
Shiva kutoka Uswizi mwaka 2014.
Kulikuwa pia na samaki kwa jina Piranha Pele kutoka Uingereza.
0 Comments