MHANDISI wa Wakala
wa barabara (TANROADS) Mkoa wa Singida,Yohannes Mbegalo anatarajia kupanda
kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa wilaya ya Manyoni,Mkoani
Singida,Juni,26,mwaka huu kutoa ushahidi katika kesi ya jinai namba 277/2017.
Katika kesi hiyo
iliyokuwa ikisikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya
Manyoni,Kiwonde,amepata uhamisho wa kwenda kufanya kazi katika Mahakama
nyingine iliyopo nje ya Mkoa wa Singida.
Mhandisi Mbegalo
atakuwa shahidi wa nne kutoa ushahidi dhidi ya watuhumiwa watatu wakazi wa
Kijiji cha Kitopeni,katika Halmashauri ya Itigi,wilayani Manyoni wanaokabiliwa
na tuhuma za kuharibu miundombinu ya barabara ya Manyoni-Itigi –Chaya na kuiba
ni kati ya mashahidi watano wanaotarajiwa kuhudhuria katika Mahakama hiyo kwa
ajili ya kutoa ushuhuda wa tukio hilo.
Watuhumiwa wa kesi
hiyo iliyopewa namba 277/2017 ni pamoja na Musa Haruna (47) mkazi wa Mtaa wa Mtimkavu Itigi,Yohana Simon (42) mkazi wa
Mtaa wa Mtimkavu Itigi pamoja na Joseph Alphonce (39) mkazi wa Mtaa wa Mlowa.
Hata hivyo katika
ushahidi uliotolewa na askari wa kikosi cha upelelezi kutoka katika Kituo cha
polisi Manyoni,Afande Chiganga Chiganga ameithibitishia Mahakama hiyo kwamba
sept,26,mwaka jana alikabidhiwa na OC CID jalada kwa ajili ya upelelezi wa
tukio hilo.
Amefafanua Chiganga
kwamba katika kesi hiyo ilionyesha kuwa kulikuwa na uharibifu wa vyuma vya
alama za barabarani vinne mali ya wakala wa barabara Tanzania (TANROADS)
vilivyoibiwa na watu wasiojulikana katika Kijiji cha Kitopeni,Halmashauri ya
Itigi.
0 Comments