Beki Pascal Wawa ameonekana akiwa mazoezini leo na wekundu wa Msimbazi katika
Uwanja wa Bocco Veterani jijini Dar es Salaam.
Taarifa za ndani
kutoka Simba zinasema tayari wameshamalizana na mchezaji huyo aliyewaji
kuicheza Azam FC.
Wawa ameonekana
kujifua leo na kikosi cha Simba katika ratiba ya mazoezi ya asubuhi kuelekea
michuano ya KAGAME inayotaraji kuanza Juni 29 2018.
Katika mazoezi hayo
yaliyofanyika chini ya Kocha Msaidizi, Masoud Djuma, Wawa ameonekana kuonesha
uzoefu na utulivu na kwenda sambamba na kile kocha wake alikuwa akimuelekeza.
Kikosi hicho kwa sasa kitakuwa kinafanya mazoezi mara moja kwa siku baada ya ile ratiba ya kujifua mara mbili kumalizika wiki iliyopita.
0 Comments