MBUNGE wa Jimbo la
Singida Magharibi Elibariki Imanuel Kingu (CCM) na wananchi wa vitongoji viwili
Sengasenga na Mrama vyenye wakazi 986 Kata ya Sepuka Wilaya ya Ikungi Mkoa wa
Singida kwa pamoja Mbunge na viongozi wao wa chama na Serikali wameshirikiana
kujenga shule mpya ya msingi kama moja ya historia ya viongozi wao na kabila la
Wanyaturu.
Imeelezwa kuwa katika
historia ya kabila la wanyaturu baada ya kutoka Abysinnia sasa Ethiopia karne
ya kumi na saba walifika Mwanza kwa kupitia Kenya wakaweka makazi Pansias
wakaondoka wakaja Singida wakaweka makazi yao kwa mara ya kwanza Sepuka eneo la
Sengasenga na baadae wakatawanyika Ikungi na Ilongero kutafuta maeneo ya kilimo
na ufugaji kama jadi yao.
Kwa upande wa viongozi
waliopo sasa madarakani Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Diwani Kata
na Sepuka, Mwenyekiti CCM Kata na Mwenyekiti na Kijiji Musimi ni Shule yao ya
kwanza kuanza kujenga kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo na ni historia
kwao katika moja ya majukumu waliopewa dhamana na wananchi.
Wanachi wa Vitongoji
hivyo viwili waliamua kutenga eneo la ekari 25 kwa ajili ya kujenga shule ya
msingi kwa kutumia fedha zao, nguvu na mali kwa kushirikiana na viongozi wa
serikali na chama (CCM) ngazi zote ili watoto wao wapate elimu kwa ukaribu.
Akizungumza na gazeti
hili juzi kwa njia ya simu Katibu wa Mbunge ofisi ya Mbunge Ikungi Bakari Omari
Munna amesema ofisi yake imetoa simenti mifuko 70 na fedha taslimu sh 700,000/=
na itaendelea kutoa misaada mingine na ushirikiano wa wananchi hao ili waweze
kukamilisha ujenzi wa shule hiyo ili mwakani wanafunzi waanze masomo.
Muna amesema ofisi yake
itasimamia kwa ukaribu wake hadi mwisho kwa malengo yote kama moja ya historia
ya Mbunge wake na hio pia itapunguza utoro rejareja kwa wanafunzi kutokana na
kufuata masomo mbali zaidi ya kilomita 8 na hio ni moja ya malengo ya ofisi
yake.
Baadhi ya wakazi wa eneo
hilo Shabani Athumani Mkuki na Mwajabu Omari Muna wameliambia gazeti hili kuwa
shule hiyo inajengwa kwa nguvu za wananchi, mbunge na viongozi wa chama na
serikali kama moja ya historia yao wakiwa madarakani na tayari madarasa mawili
yamejengwa na ofisi ya walimu kilichobakia ni lenta na upauaji, hivyo michango
inaendelea na ujenzi unaendelea.
Aidha Afisa Mtendaji kata
ya Sepuka na Diwani wa kata Yusufu Missanga wamedokeza kuwa mwakani shule hiyo
itaanza kutumika kwa sababu ujenzi wake unaendelea vizuri, michango inaendelea
na wananchi sasa wameitikia kufanya kazi hio kwa ari na moyo ili watoto wao
wapate elimu kwa faida yao kama Rais anavyoagiza.
0 Comments