Mkuu wa Taasisi ya Said Shohadaa Faundation kanda ya Afrika akiongoza Maulid kuliombea taifa mjini Singida.
SINGIDA
Waumini wa dini ya Kiislamu katika Manispaa ya Singida
wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika maulidi maalum yaliyofanyika kwenye
viwanja vya Stendi ya zamani, ambapo pamoja na kusherehekea tukio hilo tukufu,
walifanya swala maalum ya kuliombea Taifa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Mgeni rasmi katika maulidi hayo alikuwa Mkuu wa Taasisi ya
Said Shohadaa Foundation Kanda ya Afrika, yenye makao makuu yake jijini Arusha,
Sheikh Maulid Sombi, ambaye pia aliongoza swala hiyo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni kutoka nchi jirani ya Kenya pamoja na mikoa mbalimbali nchini, ikiwa ni ishara ya umoja na mshikamano wa waumini wa Kiislamu katika kuombea amani, upendo na ustawi wa Taifa.








0 Comments