Na Thomas Kiani
Singida
MFANYABIASHARA wa nyama choma minadani mkazi wa kijiji cha
Musimi Kata ya Sepuka Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida Saidi Jumanne
Mdadau(Nkimbu) (25) mwishoni mwa wiki iliyopita amenusirika kufa baada ya
kutangwa njiani usiku na kupigwa na watu wasiofahamika akitoka mnadani na
kumnyang’anya pesa zote na radio alionunua akaburuzwa mtoni na kuachwa hana
fahamu.
Akizungumza na mwandishi jana nyumbani kwa Saidi Mtoto wake
anaeitwa Ramadhani amesema siku hiyo Baba yake aliuza alizeti akanunue radio
mnadani akaendelea na kazi zake lakini hakurudi nyumbani hadi asubuhi
tuliposikia ameokotwa mtoni akiwa hoi hajitambui.
Ramadhani amesema baba yake alitangwa njiani saa 4: 00
usiku wakati wa kurudi nyumbani akapigwa na kitu kigumu shingoni, kichwani,
mgomgoni na shavuni na watu wasiofahamika akakosa fahamu pia akanyang’anywa
pesa zote za mauzo na radio aliokuwa nayo akaburuzwa mita karibu 30 hadi kwenye
korongo la mto huku akitoka damu akaachwa hadi asubuhi alipoonwa na wapiti
njia.
Akieleza juu ya hali ya majeruhi Saidi Dada yake mkubwa Tatu
Jumanne Mdandau amesema kaka yake alikuwa mtu wa kufa alipigwa akakosa fahamu, akawa
hoi akaburuzwa hadi mtoni na amelala alikotupiwa baridi yote ilimuishia akiwa
hapo korongoni hadi asubuhi akapelekwa Hospitali ya Mkoa wa Singida akiwa
hajitambui kichwa chote kilivimba kwa majeraha lakimi Mungu amempa uzima.
Tatu ameendelea kusema hapo mapokezi Hospitali ya mkoa wa
Singida walisema mmemleta wa nini huyu mtu wakati ameshakufa lakini mapigo ya
moyo wake yalikuwa bado yapo, akalazwa wodi namba tatu akawekewa dripu 12
akalishwa kwa mpira japokuwa sasa amerudishwa nyumbani lakini hali yake bado
tete.
Alisema
Aidha katika tukio hilo Mwenyekiti wa kitongoji cha
Italala mashariki Athumani Majuda amesema alipigiwa simu saa 1:30 asubuhi
kwamba Saidi (Nkimbu) ameokotwa mtoni akiwa hoi hajitambui kichwa chote
kimepigwa hawezi kusema,hawezi kuinuka na hana fahamu na alipofika alimkuta
anamajeraha kichwa chote na hajifahamu.
Majuda amesema walimchukua kwa pikipiki hadi polisi kupata
hati ya matibabu wakampeleka kituo cha afya Sepuka nao wakampeleka kwa gari
Hospitali ya mkoa wa Singida kutibiwa akiwa hana fahamu na ameelezwa baada ya
siku nne akapata ufahamu lakini hadi sasa hali yake sio nzuri japokuwa
ameruhusiwa kurudi nyumbani.
Naye Diwani wa Kata ya Sepuka Yusufu Missanga juzi aliitisha
mkutano wa hadhara kijiji cha Musimi kuzungumzia jambo hilo na yale mengine
yaliyojitokeza ilibidi wanakijiji wapige kura za siri kuwataja wahalifu na
akawaagiza polisi kuwakamata wote watakaotajwa ili wachunguzwe na kuhojiwa na
amewataka polisi kusimamia vizuri majukumu yao kuhakikisha wanalinda mali za
watu na raia zake.
0 Comments