Viongozi hawa wakiingia
katika mkutano wameonekana wenye tabasabu, na kusalimiana kwa kushikana mikono,
na baadae Kim Jong Un alimshika
bega Trumpa kisha wakaanza kuzungumza kwa msaada wa wakalimani wao.
Baadae washauri na maofisa mbalimbali wataingia kuendelea na
mkutano huku suala la nyuklia likitarijiwa kujadiliwa kwa kina na haijajulikana
bado makubaliano yatakua yapi.
Akizungumza kabla ta mkutano , katibu mkuu wa umoja wa mataifa,
Antonio Guterres amesema kuwa umoja wa mataifa utatoa msaada wowote wa
kuhamasisha makubaliono katika mkutano huo.
''viongozi wawili, wanajaribu kujadiliana jinsi ya kufikia
makubaliano ambayo yalileta sana utata mwaka jana, amani na suala la kusitisha
nyuklia ndio vinabaki kuwa lengo kuu, kama nilivyowaandikia mwezi uliopita
kutahitajika ushirikiano wa hali ya juu na kutakua na changamoto za hapa na
pale katika makubaliano, Marekani wanatakiwa kusimamia kwa vyovyote''. Alisema
Guterres.
Wakati huo huo Mcheza
kikapu wa zamani wa NBA, Dennis Rodman amefika Singapore asubuhi ya leo kwa ajili mkutano huo,
Rodman ambaye ni rafiki wa kiongozi wa Korea Kaskazini amesema kuwa anafurahia
kufika na kushuhudia mkutano huo wa kihistoria.
0 Comments