FAHAMU MABADILIKO YA MPIRA MPYA WA KOMBE LA DUNIA URUSI BAADA YA RANGI NYEUSI SASA NI NYEKUNDU



Mpira mpya utatumiwa katika mechi za hatua ya muondoano katika Kombe la Dunia nchini Urusi, shirikisho la soka duniani Fifa limetangaza.
Mpira huo uliopewa jina Telstar Mechta utachukua nafasi ya Telstar 18, mpira wa Adidas ambao umetumiwa katika hatua ya makundi.

Gozi hilo jipya lina mapambo ya rangi nyekundu, na linadaiwa kuchochewa na rangi za taifa la taifa mwenyeji, Urusi, pamoja na "joto linaloongezeka kimichezo katika hatua ya muondoano".


Mechta kwa lugha ya Kirusi maana yake ni "Ndoto".
Mpira huo utatumiwa kwa mara ya kwanza Jumamosi.
Kumekuwa na miundo mikuu 20 ya mipira tangu kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia 1930

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments