Baada
ya kuwaliza mbele ya mashabiki wa nyumbani wakiwa wenyeji wa Kombe la
Dunia 2002, Ujerumani nayo imepata kuhisi uchungu wa kutolewa Kombe
la Dunia.
Mabao
ya Son Heung-min dakika ya 96 na Kim Young-gwon dakika ya 91
yametosha kuidhalilisha Ujerumani na kuitema kutoka Dimba la Dunia.
Aidha,
Ujerumani yenye mazoea ya kuwadunisha wengine, imeadhibiwa pia
kufuatia unyama iliyowatendea Brazil 2014 kwa kuwafunga 7-1 mbele ya
mashabiki wa nyumbani.
Ujerumani
imejiunga na Ufaransa, Italia na Uhispania kuwa mabingwa waliochujwa
kutoka taji walicholenga kulitetea.
Die
Mannschaft waliingia
mchuano huo ukiwa wa mwisho, wakipigiwa upatu kwa kuwa na nafasi
nzuri ya kufuzu kutoka hatua ya makundi.
Walipojumuishwa
Kundi F, wengi walihisi ni mteremko kwa timu hiyo yenye mastaa, Mesut
Ozil na Toni Kroos.
Korea
Kusini imekuwa taifa la kwanza kutoka bara Asia Kuifunga Ujerumani.
Licha
ya matokeo hayo, Korea Kusini na Ujerumani wameelekea nyumbani huku
Sweden na Mexico wakielekea hatua ya mchujo.
Sweden
iliyomaliza wa kwanza Kundi F, inamsubiri wa pili katika Kundi E kati
ya Uswizi na Brazil.
Mexico
itakuwa na kibarua kwani itachuana na kiongozi wa Kundi E wakisaka
nafasi ya kushiriki hatua ya Robo fainali.
0 Comments