Maafisa wa kampeni wa mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump
wamepanga kumwalika kaka wa kambo wa Rais Barack Obama kuhudhuria mdahalo wa
mwisho wa urais nchini Marekani.
Maafisa
hao wamesema Malik Obama, ambaye alizaliwa Kenya, atakuwa miongozi mwa hadhira
itakayofuatilia mdahalo huo wa runinga, Bw Trump alikabiliana na mpinzani wake
wa chama cha Democratic Hillary Clinton.
Malik,
aliambia gazeti la New York Post kwamba ana furaha isiyo na kifani kwamba
atahudhuria mdahalo huo.
"Trump
anaweza kuirejeshea Marekani fahari yake tena," amesema, kwa mujibu wa
shirika la habari la AP.
Wagombea wamekuwa wakitumia wageni kwenye
midahalo kama njia ya kuwakabili wapinzani wao.
0 Comments