SHILINGI MIL8.5 ZATUMIKA KUJENGA UWANJA WA KIKAPU ITIGI - SINGIDA



Na,Jumbe Ismailly ITIGI     

HALMASHAURI ya Itigi,Wilayani Manyoni,Mkoani Singida imetumia zaidi ya shilingi milioni 8.5 kujenga uwanja wa mchezo wa basketball katika shule ya sekondari ya mchepuo wa michezo Itigi ili kuboresha miundombinu ya viwanja vilivyopo katika shule hiyo pamoja na kuweza kuhodhi mashindano ya UMISSETA yanayofanyika Kimkoa katika Halmashauri hiyo.

Ofisa michezo wa Halmashauri ya Itigi,Wilayani Manyoni,Mkoani Singida,Erasto Lazaro aliyasema hayo katika mahojiano maalumu na kituo hiki kilichotaka kufahamu maudhui ya Halmashauri hiyo kujenga uwanja huo wa kisasa katika shule hiyo.

Alifafanua ofisa huyo kwamba kutokana na shule hiyo ya sekondari Itigi kuwa shule pekee wilayani Manyoni ya mchepuo wa michezo,hivyo waliona ni busara kuboresha miundombinu ya michezo shuleni hapa sambamba na kuiwezesha Halmashauri kuhodhi mashindano ya UMISSETA yanayoendelea kimkoa katika viwanja hivyo.
.
Hata hivyo Lazaro alisema Halmashauri hiyo ina mipango endelevu juu ya kujenga viwanja vya michezo mingine kwa kutumia wadau pamoja na watu wengine ambapo hata hivyo wataendelea pia kuboresha viwanja vya michezo mingine.

Kuhusu uvamizi wa viwanja,ofisa michezo huyo alikiri kwamba tatizo hilo bado lipo katika Halmashauri hiyo,hususani kwenye maeneo ya wazi bado wananchi wanaendelea kuyavamia.

Kwa mujibu wa Lazaro jitihada zinaendelea kufanyika kwa kuwatumia maafisa ardhi kwa ajili ya kuyapima na kuyaandalia hati miliki ili yaweze kuachwa na yaendelezwe kwa ajili ya matumizi ya viwanja.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments