KIJANA mmoja mkazi wa kijiji cha
kintandaa kata ya Mtunduru, wilaya ya Ikungi mkoani Singida Hashimu Jumanne
(16) amekutwa amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia
kamba ya chandarua anayotumia mama yake kufungia kuni.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili
juzi katika kijiji hicho mama yake mzazi Mwasiti Hasaani Athumani amesema tukio
la kujinyonga mwanae lilitokea Ijumaa 25/5/2018 asubuhi na yeye akamgundua saa
7:00 mchana kwamba amejinyonga kwenye mti uliopo ndani ya shamba lao wakati
akimtafuta aende kula na wenzake.
Mwasiti alisema siku hio asubuhi yote
Hashimu alikuwa anachota maji ya kutumia nyumbani kwa baiskeli hadi saa 4:00
asubuhi yeye akaenda kukata kuni na aliporudi akaanza kuwapikia chakula hadi
saa 6:00 mchana akaanza kumtafuta ili aje kula akamkosa.
Aliendelea kueleza yeye aliporudi kwenye
kuni alimkuta Hashimu amechukua msumari mkubwa anatoboa matundu ukutani ili
awajengee njiwa zake kibanda lakini alimkataza kutoboa ukuta akamnyanganya
msumari huo hali hiyo ilisababisha mabishano makali kati yao, hapo
hawakuonana tena hadi alipomkuta amekufa juu ya mti.
Aidha afisa Mtendaji wa kijiji hicho cha
Kintandaa Zuhura Amani Kiula amesema amepata taarifa hiyo saa 8:00 mchana akiwa
ofisini kwake kutoka kwa soa Shabani kwamba katika eneo lake kijana mmoja
amekufa kwa kujinyonga.
Zuhura amesema alifika akafanya
mahojiano na wazazi wake pamoja na ndugu zake kujua vyanzo vyake lakini hakuona
jambo gumu lililojitokeza kuhusiana na tukio hilo lililomfanya kijana Hashimu
achukue maamuzi magumu hadi afike hatua ya kujinyonga.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji kata ya
Mtunduru Adamu Jambau amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo la kujinyonga kwa kijana
huyo katika kijiji hicho na katika mahojiano na wazazi wake hakuona tatizo gumu
ila tu marehemu hakuelewa lugha na mama yake juu ya kujenga banda la njiwa
zake.
Polisi walifika wakafanya uchunguzi na
mahojiano na wazazi juu ya tukio hilo na baadae na viongozi wa Kijiji wakabaini
hakuna jambo gumu lililomfanya marehemu afikie maamuzi hayo magumu zaidi ya
malumbano na mama yake wako huru marehemu azikwe na hakuna mtu aliyechukuliwa
na polisi kwa mahojiano.
0 Comments