TIMU ya Singida United imemthibitisha kuwa Mrundi Etienne
Nayiragijje kuwa kocha wake mpya, akichukua nafasi ya Mholanzi, Hans van der
Pluijm anayeondoka.
Pluijm anaondoka Singida United baada ya msimu mmoja, akiongea
na Katemanablog katibu mkuu wa Singida united Abdulhaman Sima amema kuwa Coach
Ndayiragiji amekwishawasili mkoni Singida mapema kabla ya mchezo wa VPL dhidi
ya Simba na alikuwepo jukwaani akitazama
mchezo huo ambapo Singida United ilipoteza kwa 1-0 katika wanjawake wa Namfua.
Sima amesema kuwa Mholanzi Hans van pluijm aliuomba uongozi wa
Singida united kumuita mapema mrithi wake Mrudi Ndayiragiji ili amkabithi
mikoba yake mapema baada ya mchezo wa fainali ya Azam Sports Federatin Cup
(ASFC) utakao chezwa jijini Arusha na baada ya mchezo huo timu itaelekea jijini
Nairobi katika michezo ya Super spots.
Ndayiragijje ambaye amekwishaachana na Mbao FC aliyoiongoza kwa
misimu miwili akitokea kwao Burundi.
Msimu uliopita, Ndayiragijje pamoja na kunusurika kuishusha Mbao
FC, lakini aliiwezesha kufika fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) ambako ilifungwa na Simba
SC 2-1 Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Na msimu huu, Ndayiragijje aliingia kwenye mtafaruku na uongozi
wa klabu hiyo ya Mwanza baada ya mzunguko wa kwanza tu wa Ligi Kuu na kuondoka,
nafasi yake ikichukuliwa na mchezaji wa zamani wa Pamba SC, Fulgence Novatus.
0 Comments