Washambuliaji Lionel Messi, Sergio
Aguero, Paulo Dybala na Gonzalo Higuain wamejumushwa katika kikosi cha
wachezaji 23 watakaoiwakilisha Argentina kwenye kombe la dunia nchini Urusi.
Lakini mfungaji bora zaidi wa ligi ya Serie A mshambuliaji wa
Inter Milan Mauro Icardi ameachwa nje.
Aguero anajiunga na wachezaji wengine watano wa Premier League
akiwemo wanayecheza pamoja huko Manchester City Nicolas Otamendi.
Argentina wataaza mechi za Kombe Dunia dhidi ya Iceland tarehe
16 Juni kabla ya mechi zingine dhidi ya Croatia na Nigeria katika kundi D.
Nusura watupwe nje ya Kombe la Dunia lakini hat-trick ya
mshambuliaji wa Barcelona Messi iliwaokoa wakati wa mechi yao ya mwisho ya
kufuzu.
Kikosi kamili cha Argentina
Walinda lango: Sergio Romero (Manchester United),
Willy Caballero (Chelsea), Franco Armani (River Plate).
Walinzi: Gabriel Mercado (Sevilla), Federico Fazio
(Roma), Nicolas Otamendi (Manchester City), Marcos Rojo (Manchester United),
Nicolas Taglafico (Ajax), Javier Mascherano (Hebei Fortune), Marcos Acuna
(Sporting Lisbon), Cristian Ansaldi (Torino).
Viungo wa kati : Ever Banega (Sevilla), Lucas
Biglia (AC Milan), Angel Di Maria, Giovani Lo Celso (wote wa Paris St-Germain),
Manuel Lanzini (West Ham), Cristian Pavon (Boca Juniors), Maximiliano Meza
(Independiente), Eduardo Salvio (Benfica).
Washambuliaji: Lionel Messi (Barcelona), Gonzalo
Higuain, Paulo Dybala (both Juventus), Sergio Aguero (Manchester City).
0 Comments