Na,Jumbe Ismailly Manyoni
HALMASHAAURI ya wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida imepata kibali cha kutumia shilingi milioni 920 kwa ajili ya kuongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kutoka asilimia 24 iliyopo sasa hadi kufikia asilimia 52.
Akizungumza na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Kaimu Mkuu wa wilaya ya Manyoni,Bwana Miraji Mtaturu amesema suala la upatikanaji wa maji safi na salama katika Mji wa Manyoni bado ni kitendawili kinachotakiwa kipatiwe ufumbuzi wa madhubuti na wa haraka zaidi.
Aidha Bwana Mtaturu ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Ikungi amebainisha kuwa kati ya kiasi hicho cha fedha,shilingi milioni 200 zimeshatumika kuwalipa SUWASA ili waanze kuchimba visima pamoja na kufunga pampu.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa wilaya ili kufanikisha upatikanaji huo wa maji,wameomba pia shilingi milioni 300 kupitia force account ili iweze kufanikisha azma ya kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kufikia asilimia 52.
Akifunga mkutano huo wa siku ya kwanza wa Baraza la madiwani,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Bwana Moses Matonya ameonyesha kukerwa na hatua zilizochukuliwa za kuifunga shule ya sekondari Kilimatinde kutokana na kutokuwa na matundu ya vyoo vya kutosha.

0 Comments