Na Kutoka Manyoni
WAKAZI
wawili wa Mji mdogo wa Itigi,wilayani Manyoni,Mkoani Singida Hasani Masare na
Juma Salumu wanasshikiliwa na polisi wilaya ya Manyoni kwa tuhuma za kupatikana
na mazao ya misitu aina ya magogo 423 ya miti mbali mbali
yasiyokuwa na kibali cha uvunwaji wala usafirishwaji kutoka Kaliua,wilayani
Mapanda,Mkoa wa Katavi hadi katika Kijiji cha Damwelu,kata ya Ipande,wilayanai
Manyoni.
Mafanikio
ya kukamatwa kwa wakazi hao yalitokana na ushirikiano kati ya wananchi waliotoa
taarifa,Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) pamoja na polisi wilayani Manyoni na
kwamba magogo hayo yaliyokuwa yakiingizwa usiku kwenye mashamba hayo ya Mbunge
ni ya miti aina ya mitundu na mininga.
Akithibitisha
kukamatwa kwa wakazi hao,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Itigi,Bwana Pius
Luhende amesema baada ya kupata taarifa hizo za kufichwa kwa mazao hayo aina ya
magogo alilazimika kuwatuma maafisa wake wa idara ya misitu usiku wa kuamakia
okt,10 na wakati wakiwa kwenye doria ndipo watuhumiwa hao walipofika na kukiri
kwamba walikuja kuangalia mali yao hiyo.
Aidha Bwana
Luhende ameweka bayana pia kwamba kufuatia maelezo yao hayo ndipo waliwekwa
chini ya ulinzi na baada ya kuhojiwa tena waliikana mali hiyo kuwa siyo
yao na kumtaja mmiliki wa magogo hayo yaliyokutwa kwenye shamba la Mbunge wa
jimbo la Manyoni Magharibi,Bwana Yahaya Masare kuwa ndiye mali yake.
Naye
Mwenyekiti wa Kijiji cha Damwelu,Bwana Masaanja Lugemela amesema hakuwa
na taarifa yeyote ile juu ya uingiaji wa magogo hayo ila baada ya kupigiwa simu
saa nane usiku na kaimu afisa mtendaji wake wa Kijiji kwamba kwenye mbuga ya
Mzee Danieli kuna mzigo mkubwa wa magogo ambao haukuwa ukifahamika ni wa nani
na kumuomba waende wakauone.
Katika
utetezi wake kuhusu kutajwa na watuhumiwa kuwa ndiye mmiliki halali wa magogo
hayo kutokana na kuwepo kwenye shamba lake,Mbunge wa jimbo la Manyoni
Magharibi,Bwana Yahaya Masare licha ya kukiri kuwa eneo hilo ni mali yake vile
vile amekiri pia kwamba Kampuni iliyosafirisha magogo hayo ni ya vijana wake
hivyo anaweza kubeba dhamana ya tuhuma hizo.
Zoezi la
kuhakiki idadi ya magogo yanayomilikiwa na Mbunge wa jimbo la Manyoni Magharibi
lililoanza Jumanne ya wiki hii pamoja na vibali vilivyokuwa vikitumika
kusafirishia magogo hayo lilitarajiwa kuendelea tena leo Jumatano ili
kujiridhisha iwapo vinakidhi vigezo vya kisheria.
0 Comments