Waziri Dr Charles Tizeba akiongea katika gwalide la mifugo Nane nane mijini Dodoma |
WAZIRI
wa kilimo na Mifugo nchini Dk Charles Tizeba amesema kwamba taifa kwa
sasa linajitosheleza kwa chakula kwa asilimia 120 tu.
Waziri huyo
alisema hayo katika mashindano ya mifugo katika viwanja maonesho ya
Nanenane nzuguni mkoanji hapa.
Waziri tizeba
alisema tathmini iliyofanyika inaonesha kwamba Tanznia inajitosheleza kwa
chakula kwa asilimia 120
“Chakula
kilichopo kinatutosha.Watanzania wale wenye tabia ya kuuza chote na kwenda kwa
wakuu wa mikoa au wilaya na kusema hawana chakula taratibu huo haupo.
“Wako watu
wanakiuka utaratibu wanauza chakula chote halafu wanaliamsha ili watu wote
wakose usingizi” alisema Dk Tizeba.
Alisisitiza
haja ya wananchi kuacha tabia ya kuuza chakula chote kwani kufanya hivyo ni
kuitia familia katika matatizo makuhbgwa.
“Utaona mtu
ana gunia nne halafu anazipeleka zote sokoni kwa kutegemea kuliamsha mbele ya
safari, halitaamka.” alisisitisza Dk Tizeba.
Aidha
aliwataka wananchi kuzingatia maelekezo yaliyotolewa kwa wale wanaotaka
kusafirisha mazao nje ya nchi kwamba ni lazima kwanza waongeze thamani.
Pia alisema
kwamba serikali inajitahidi kushusha gharama katika kilimo na hivi karibuni
ilifuta tozo mbalimbali 108 katika kilimo, uvuvi na mazao ya mifugo baada ya
kubaini kodi zinaongeza bei ya bidhaa ikiwa ni pamoja na kuondoa kodi
katika mbolea na viuatilifu ili iwe rahisi kwa mkulima kuzalisha kwa kutumia
teknolojia ya kisasa.
Aidha waziri
huyo alisema serikali itatangaza bei mpya ya mbolea kwa lengo la kuachana na
bei holela ili kila mwananchi amudu bei hiyo.
“Tumeanza
kuchukua hatua kuhakikisha bei ya mbolea kila mtu anamudu, mambo ya ruzuku moja
kwa moja kwenye mbolea tunakwenda kuachana nayo, “ alisema Dk Tizeba.
Awali Katibu
Mkuu wizara ya Kilimo na mifugo Dk Mary Mashingo alisema wananchiwananchi
wamekuwa wakielimishwa juu ya mbinu mbalimbali za kilimo na ufugaji.
Mfugaji mwingine kutoka Manyoni akiwa na Kanyankole wake katika gwalide hilo la mashindano. |
anakilo 800 ng'ombe kutoka Dodoma na umri wa maiaka 4 |
wapambe wa Chifu wakisafisha njia kabla ya kuingia. |
Huyu Ng'ombe anatokea Manyoni ni Chifu alivyoingia alikaribishwa kama mfalme kwa ngoma za asili. |
0 Comments